11 February 2014


Serikali ina mpango wa kujenga mji wa kisasa katika eneo la Usa River lililoko kilomita 15 kutoka mji wa kitalii wa Arusha ulioko kaskazini mwa nchi hiyo.

Hayo yamesemwa jana na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la nyumba Tanzania NHC, Nehemiah Mchechu. Mchechu amepongeza juhudi za serikali katika kudhibiti wingi wa watu kwenye mji wa Arusha. Amesema Shirika hilo tayari limenunua heka 300 za ardhi kwa gharama ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 3. Ameongeza kuwa, wataalam kutoka wizara ya ardhi, nyumba, na maendeleo ya makazi wameshawasili mjini Usa River ili kuangalia jinsi mji huo wa kisasa utakavyojengwa. Mchechu amesema mji huo wa kisasa utakuwa na mahitaji yote muhimu kama maduka makubwa, makazi ya watu, huduma za afya, shule, na ofisi.

Hata hivyo, Mchechu hakueleza wazi ujenzi wa mji huo utagharimu kiasi gani.


Wakati huo huo, serikali ya imedhamilia kujenga uwanja wa ndege karibu na mbuga ya Serengeti Tanzania.

Mwanaharakati wa uhifadhi kutoka marekani ambaye pia ni mafanyibiashara mashuhuri anashirkiana na Serikali ya Tanzania kujenga uwanja wa kisasa wa ndege karibu na hifadhi ya wanyama ya Serengeti.

Paul Jones, ambaye amewekeza fedha nyingi kwenye sekta ya utalii nchini Tanzania amekubali kufadhili ujenzi wa uwanja huo ambao utarahisisha uchukuzi wa watalii wanaotembelea hifadhi ya Serengeti.

Zaidi ya dola milioni 30 tayari zimetengewa kwa uwanja huo.

Watalii wanaotembelea Serengeti hulazimika kutumia uwanja wa Arusha ambao uko mbali,

Mbunge wa eneo la Serengeti Dokta Kebwe S Kebwe alisema ujenzi wa uwanja huo kwenye mji wa Mugumu utaanza mwaka huu.

Utakapokamilika uwanja huo utatua ndege zenye abiria 60

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!