28 August 2012

Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto kuingilia kama kuna sheria inayomruhusu Mtoto na Mama yake mzazi kuweza kuishi kindoa.
Hayo yamebainika katika Kijiji cha Namabengo Wilaya ya Namtumbo baada ya Joseph Mapunda kuweza kuishi na Mama yake kindoa kwa miaka 10 mfululizo.
Joseph Mapunda amesema ameweza kuishi na kushiriki tendo la ndoa na  Mama yake Mzazi baada ya yeye kukubaliana na mama yake mzazi kuishi mke na mume.
Alipoulizwa mama anayefahamika kwa jina la Kondrada Ngonyani alikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mume wake ambaye ni Mtoto wake Joseph Mapunda.
Umati wa watu uliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma watu wapatao 400 wameomba Serikali ichukue mkondo wa Sheria kuvunja ndoa hiyo.
Kwa Mkoa wa Ruvuma hii ni mara ya kwanza mtoto wa kiume kutembea na mama yake
 mzazi.
 stori kutoka..www,ruvumayetu.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!